Lisa College Lisa College Lisa College
bg-banner
shape

Kuhusu Sisi

Kuhusu Sisi

Jenga Future Yako na Lisa College!

Je, unatamani kujiajiri au kupata ajira kupitia ujuzi wa vitendo? Lisa College ndiyo sehemu sahihi kwa ajili yako! Sisi ni chuo kilichosajiliwa rasmi na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kwa namba ya usajili REG/NACTVET/1042P.

Kwa zaidi ya miaka, Lisa College imekuwa ikitoa mafunzo ya kitaalamu na ya vitendo kwa vijana na watu wazima, kuwawezesha kujenga mustakabali bora kupitia ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira la ndani na nje ya nchi.

icon

Dira Yetu (Our Vision)

Kuwa kitovu kikuu cha mafunzo ya ujuzi wa vitendo nchini Tanzania, kinachozalisha wataalamu wabunifu na wenye ushindani mkubwa katika sekta ya urembo, ushonaji, ususi na huduma.

icon

Dhima Yetu (Our Mission)

Kutoa mafunzo bora ya amali kwa kutumia vifaa vya kisasa na wakufunzi wenye uzoefu, ili kumuwezesha kila mwanafunzi kupata ujuzi thabiti utakaomsaidia kujiajiri na kuajiriwa kwa urahisi.

icon

Usajili Rasmi

Chuo kimesajiliwa na kutambuliwa na Serikali ya Tanzania kupitia NACTVET (REG/NACTVET/1042P). Tunatoa vyeti vinavyotambulika kitaifa na kimataifa.

Lisa College
Lisa College

2k+

Wahitimu Wetu

Lisa College
Mafunzo Yetu

Kozi Zinazotolewa

Lisa College inatoa mafunzo ya kitaalamu katika nyanja mbalimbali za urembo, ushonaji, na huduma. Mafunzo yetu yameundwa kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na mahitaji ya soko la ajira.

Urembo

Makeup na Cosmetology

Makeup za aina zote, facial na full body massage, na huduma za urembo kwa viwango vya kimataifa.

Ususi

Ususi wa Nywele

Hair dressing, styling, dreadlocks, na mitindo yote ya kisasa na ya kitamaduni ya nywele.

Kucha

Utengenezaji wa Kucha

Mafunzo ya kitaalamu ya utengenezaji na upambaji wa kucha kwa kutumia vifaa vya kisasa.

Mapambo

Mapambo ya Kumbi

Ubunifu na upambaji wa kumbi za sherehe, harusi, na matukio mbalimbali kwa weledi wa hali ya juu.

Ushonaji

Ushonaji na Designing

Mafunzo ya ushonaji wa mavazi ya kisasa, ubunifu wa nguo za harusi, na fashion design kwa viwango vya juu.

Keki

Utengenezaji na Upambaji wa Keki

Mafunzo kamili ya kuoka mapambo ya keki kwa ajili ya harusi, sherehe na biashara ya mikate.

Massage

Facial & Full Body Massage

Mafunzo ya kitaalamu ya massage ya uso na mwili mzima kwa kutumia mbinu za kisasa za tiba na urembo.

Henna

Henna na Piko

Mafunzo ya sanaa ya henna na piko kwa ajili ya mapambo ya mikono, miguu, na matukio mbalimbali.

Harusi

Ubunifu wa Nguo za Harusi

Mafunzo maalum ya ubunifu, ushonaji na upambaji wa nguo za harusi za kisasa na za kitamaduni.

Kwa Nini Sisi

Kwa Nini Uchague Lisa College?

icon

Usajili Rasmi

Tunatambuliwa na Serikali kupitia NACTVET. Vyeti vyetu vinatambulika kitaifa.

icon

Matawi Mengi

Dar es Salaam (Tabata Kinyerezi, Gongo la Mboto, Mbagala, Songas) na Mwanza (Kishili).

icon

Vifaa vya Kisasa

Wanafunzi wanajifunzia vifaa halisi vinavyotumika kazini kwa viwango vya kimataifa.

icon

Ada Nafuu

Tunatoa fursa ya kulipa ada kwa awamu ili kila mmoja aweze kumudu.