Lisa College Lisa College Lisa College
bg-banner
shape

Wakufunzi Wetu

Wakufunzi Wetu

Wakufunzi Wenye Uzoefu na Weledi

Lisa College inajivunia kuwa na wakufunzi wenye uzoefu mkubwa na weledi wa hali ya juu katika nyanja mbalimbali za urembo, ushonaji, ususi na huduma. Wakufunzi wetu wamepitia mafunzo maalum na wana ujuzi wa kutosha kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu bora na ya vitendo.

Kila mwakufunzi ana utaalamu wake maalum, akitoa mwongozo wa kitaalamu kwa wanafunzi ili kuwasaidia kufikia malengo yao ya kazi na ujasiriamali.

Utaalamu Wetu

Wakufunzi Kwa Kila Kozi

Chini ni orodha ya wakufunzi wetu kwa kila kozi wanazozifundisha. Kila mwakufunzi amebobea katika fani yake na ana uzoefu wa miaka mingi.

icon

Wakufunzi wa Makeup

Urembo na Cosmetology

Wakufunzi wetu wa makeup wamebobea katika makeup za aina zote: sherehe, harusi, picha, na matukio mbalimbali. Wanafundisha mbinu za kisasa za kujipamba kwa viwango vya kimataifa.

icon

Wakufunzi wa Ususi

Hair Dressing na Styling

Wakufunzi walio bobea katika ususi wa kisasa na wa kitamaduni, ikiwa ni pamoja na braids, dreadlocks, styling, na mitindo yote ya nywele kwa wanawake na wanaume.

icon

Wakufunzi wa Ushonaji

Tailoring na Fashion Design

Wakufunzi wenye ujuzi wa ushonaji wa mavazi ya kisasa na ya kitamaduni, ubunifu wa nguo za harusi, na fashion design kwa viwango vya juu vya kitaalamu.

icon

Wakufunzi wa Kucha

Nail Art na Utengenezaji

Wakufunzi wetu wa kucha wamebobea katika utengenezaji na upambaji wa kucha kwa kutumia vifaa vya kisasa, ikiwa ni pamoja na nail art, acrylic na gel.

icon

Wakufunzi wa Mapambo

Event Decoration

Wakufunzi wenye uzoefu wa kupamba kumbi za sherehe, harusi, na matukio mbalimbali. Wanafundisha mbinu za ubunifu na upambaji kwa weledi.

icon

Wakufunzi wa Keki

Baking na Cake Decorating

Wakufunzi walio bobea katika kuoka na kupamba keki za aina mbalimbali kwa ajili ya harusi, sherehe na biashara ya mikate kwa viwango vya kitaalamu.

icon

Wakufunzi wa Massage

Facial na Body Massage

Wakufunzi wenye weledi katika massage ya uso na mwili mzima, wakitumia mbinu za kisasa za tiba na urembo kwa ajili ya afya na starehe.

icon

Wakufunzi wa Henna na Piko

Henna Art

Wakufunzi walio bobea katika sanaa ya henna na piko, wakifundisha mbinu za kisasa na za kitamaduni za kupaka henna kwa ajili ya mapambo ya mikono, miguu na matukio.

icon

Wakufunzi wa Dreadlocks

Dreadlocks Specialist

Wakufunzi wenye utaalamu wa kutengeneza na kutunza dreadlocks kwa viwango vya kitaalamu, wakifundisha mbinu za kisasa na za kitamaduni za kutengeneza nywele za Dreadlocks.

Sifa Zetu

Kwa Nini Wakufunzi Wetu ni Bora

icon

Uzoefu wa Miaka Mingi

Wakufunzi wetu wote wana uzoefu wa miaka mingi katika fani zao, wakiwa na rekodi ya kutoa mafunzo bora kwa wanafunzi wengi waliofaulu.

icon

Ufundishaji wa Vitendo

Wanafunzi wanajifunza kwa vitendo kila siku chini ya uangalizi wa wakufunzi wenye weledi, kwa kutumia vifaa halisi vya kazi.

icon

Ushauri wa Kazi

Wakufunzi wetu hutoa ushauri na mwongozo wa kazi kwa wanafunzi, kuwasaidia kujiajiri au kupata ajira baada ya kuhitimu.

icon

Mafunzo Endelevu

Wakufunzi wetu hupitia mafunzo endelevu ili kubaki na mbinu za kisasa na kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu inayoendana na soko.

Jiunge Nasi Leo!

Jifunze kutoka kwa wakufunzi wenye weledi na uzoefu. Soma leo, fanikiwa kesho.

📞 Piga simu au WhatsApp: 0763 493 716